KIJANA AFUNGA NDOA NA WANAWAKE WAWILI KWA WAKATI MMOJA - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 27 June 2018

KIJANA AFUNGA NDOA NA WANAWAKE WAWILI KWA WAKATI MMOJA

Mohamed na wake zake wawili


Kijana mmoja raia wa Somalia ambaye alioa wanawake wawili usiku mmoja ameambia BBC kwamba atawashawishi wanaume wengine kufanya hivyo.

Bashir Mohamed anasema kuwa aliwachumbia wanawake wote kwa takriban miezi minane na kuwashawishi kufunga ndoa naye.

''Nilikuwa nikiwaleta nyumbani wote pamoja'', aliambia BBC.

''Nilikuwa nikiwaambia wazi wote wawili kwamba nawapenda. Waliridhika'' , aliongezea.

''Umuhimu wa kuwaoa wote wawili wakati mmoja ni kwamba hawangekuwa na wivu na kwamba watajua tangu awali kwamba wamekuwa katika ndoa za uke wenza'', alisema bwana Mohammed.

Alioa wanawake wawili kwa sababu alihitaji watoto wengi.

''Nitawashawishi wanaume wengi pia kufuata nyayo zangu iwapo wana uwezo'', alisema Mohamed.

Ndoa za wake wengi ni halali katika utamaduni nchini Somalia lakini sio jambo la kawaida kuoa wanawake wawili wakati mmoja, kulingana na mwandishi wa BBC Mohamed Mohamed.

''Imetokea mara kadhaa katika miaka ya nyuma , ikiashiria kwamba huenda sasa ikawa mtindo mpya'', aliongezea.

Bwana Mohamed aliwaoa wanawake hao wawili , Iqra na Nimo, katika kijiji cha Sinai katika jimbo lililojitenga la Somaliland mnamo tarehe 22 mwezi Juni.

Chanzo-BBC

No comments:

Post a Comment