Kichaa Ateketeza Ofisi ya Ridhiwani - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 18 June 2018

Kichaa Ateketeza Ofisi ya Ridhiwani

Ofisi ya Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete jana jioni imeteketea kwa moto na kusababisha uharibifu mkubwa ambao bado thamani yake haijafahamika lakini jengo lote limeteketea.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shanna amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa kuna mwanamke aliyedhaniwa kuwa na matatizo ya akili ambaye alikusanya taka na kuzichoma nje ya ofisi, ambapo upepo ulipelekea moto kushika jengo la ofisi hizo.

“Kuna Mwanamke kichaa alikuwa na moto nje ya ofisi, upepo ulipokuja ulisukuma moto ukashika jengo, ambapo kikosi cha zimamoto na uokoaji kwa kushirikiana na wananchi, walifanya kazi ya kuuzima lakini tayari ulikuwa umeteketeza jengo zima na mali chache ziliokolewa ”, amesema Kamanda Shanna.

Aidha Kamanda Shanna amesema kuwa hasara iliyotokana na moto huo bado Mh. Ridhiwani anapiga hesabu na atakapokamilisha atatoa taarifa rasmi. Msikilize Kamanda Shanna hapo chini

No comments:

Post a Comment