Kauli Aliyoitoa Leo Rais Magufuli kwa Viongozi wa Dini Kuhusu Matamko Yao - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 12 June 2018

Kauli Aliyoitoa Leo Rais Magufuli kwa Viongozi wa Dini Kuhusu Matamko Yao

Rais Dkt. John Magufuli amewataka viongozi wa dini nchini Tanzania kuacha tabia ya kuwatafuta wasemaji wa dini zao bali wanapaswa wazungumze wao wenyewe kitu wanachotaka kukifikisha kwa waumini wao ili kuweza kunusuru chumvi za watu watakaotumwa kuwazungumzia.


Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Juni 12, 2018 wakati alipokuwa anafanya ukaguzi wa Msikiti Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam kwa kupitia mfadhili Mfalme Mohammed wa sita kutoka Morocco.

"Mkishakuwa na wasemaji wengi katika masuala ya dini hata yale mnayoyasema yanakosa maana na mara nyingi huwa yanakosa muelekeo na wasikilizaji hawataelewa kuwa hayo yanayosemwa yanatoka kwa viongozi wa dini au na wengine waliotumwa na wanaotumwa mara nyingi wanapenda kuweka chumvi kwa manufaa yao binafsi", amesema Rais Magufuli.

Pamoja na hayo, Magufuli ameendelea kwa kusema "panapozungumzwa neno lolote linalohusu masuala ya dini au ushauri wowote unaohusika na dini, unapaswa uzungumzwe na watu wa dini wenyewe kama ni masheikh azungumze Mufti, kama Mchungaji azungumze Mchungaji msitafute wasemaji kwa niaba yenu, mtakuwa mnatupoteza pabaya".

Mbali na hilo, Rais Magufuli amewahakikisha viongozi wa dini zote nchini kuendelea kushirikiana nao kwa hali na mali kwa kuwa serikali haina dini.

"Napenda kuwaahidi viongozi wa dini zote kwamba serikali yangu itaendelea kushirikiana na dini zote na niendelee kuwaomba viongozi wa dini msiwe na wasemaji ambao sio viongozi wa dini. Mnapokuwa viongozi wa dini halafu mkawatumia wasemaji ambao sio viongozi wa dini labda ni wanasiasa, mtakuwa mnachanganya dini na siasa ambacho ni kitu kibaya sana", amesisitiza Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amepewa ahadi na wakandarasi wa ujenzi wa msikiti huo ambao utakuwa unabeba zaidi ya watu elfu nane (8,000) kuwa unatarajiwa kukamilika mwaka 2019 kati ya mwezi Aprili au Mei
Chanzo: EATV

No comments:

Post a Comment