JeWajua - Wajerumani hawajawahi kutolewa kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Dunia, Je leo? - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 27 June 2018

JeWajua - Wajerumani hawajawahi kutolewa kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Dunia, Je leo?Germany 🇩🇪 vs South Korea 🇰🇷 .
South Korea 🇰🇷 watakuwa bila ya nahodha wao Ki Sung-yueng, ambaye amepata majeruhi kwenye misuli ya nyuma ya mguu.
Coach Shin Tae-yong anafahami timu yake inahitaji ushindi na hivyo lazima achague timu ambayo itacheza mchezo wa kushambulia zaidi.
.
Germany watakuwa wanamkosa Jerome Boateng ambaye ana kadi nyekundu aliyoipata vs Sweden, lakini beki mwenzie wa Bayern Mars Hummels yupo fiti kurejea kikosini baada ya kuukosa mchezo uliopita.
.
Midfielder Sebastian Rudy hatocheza leo baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa pua baada ya kuumizwa katika mtanange vs Sweden.
.
Nini wanahitaji Ujerumani ili kufuzu
.
Joachim Low na vijana wake wanahitaji ushindi ili kutimiza pointi 6 huku wakiiombea Sweden ipate matokeo yoyote ambayo hayatowazidi kitakwimu zozote.
:
#Takwimu: Mechi mbili kati ya 3 baina ya timu hizi zimechezwa katika World Cup - Wajerumani wakishinda zote mbili (3-2 mwaka 1994 & 1-0 mwaka 2002). Ushindi pekee wa South Korea dhidi ya Ujerumani ulikuwa katika mchezo wa kirafiki mwaka 2004.

No comments:

Post a Comment