Inasikitisha! Ambaka Mama Yake Mzazi Kisha Kumchinja na Panga Hadi Kufa - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 21 June 2018

Inasikitisha! Ambaka Mama Yake Mzazi Kisha Kumchinja na Panga Hadi Kufa

Mkazi wa mtaa wa Wang'waray mjini Babati mkoani Manyara anashikiliwa na polisi akidaiwa kumbaka mama yake mzazi, kisha kumuua kwa kumchinja akitumia panga.Inadaiwa kuwa mkazi huyo ambaye anaishi nyumba moja na mama yake alifanya tukio hilo akiwa amelewa baada ya kuvuta bangi na kurudi nyumbani ambapo alimkuta mama yake pia amelewa pombe za kienyeji.Akizungumza  leo Juni 21 na Mwananchi, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Asia Ramadhani alisema mwanamke huyo alifariki dunia Juni  19 saa 4 usiku akiwa nyumbani kwake katika mtaa huo.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Agustino Senga amesema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 51, alifariki dunia kwa kukatwa shingoni na kitu chenye ncha kali baada ya kubakwa."Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi kabla ya kufanyika kwa mazishi," amesema Kamanda Senga.

No comments:

Post a Comment