ICC yatoa hukumu dhidi ya aliyekuwa Makamu wa Rais - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 9 June 2018

ICC yatoa hukumu dhidi ya aliyekuwa Makamu wa Rais


Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), imemuondolea Makamu wa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Jean Pierre Bemba makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu ambayo alitiwa hatiani.

Pierre alikuwa anatumikia kifungo cha miaka 18 jela kutokana na makosa hayo ambapo alitiwa hatiani mwezi Machi 2016 kwa makosa ya uhalifu, uliotokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002, na 2003.


Mahakama hiyo imetoa uamuzi huo kufuatia rufani aliyoiwasilisha kupinga hukumu hiyo, ambapo uamuzi wa Mahakama umepokelewa kwa shangwe na wafuasi wake waliokuwepo ukumbi wa Mahakama.

Pierre alilaumiwa kwa kushindwa kuwazuia waasi wake wasiwaue na kuwabaka watu, lakini Jaji Christine Van den Wijngaert, wa ICC amesema mwanasiasa huyo hawezi kulaumiwa kwa vitendo vya waasi..

No comments:

Post a Comment