Huyu Ndiye Mwanamume Aliyeanzisha Kombe la Dunia - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 19 June 2018

Huyu Ndiye Mwanamume Aliyeanzisha Kombe la Dunia

Huku mashindano maarufu zaidi ulimwenguni yakiendelea Urusi, ni wapenzi wachache sana wa kandanda wanaojua chanzo cha mashindano ya Kombe la Dunia.

Mashindano hayo yalianzishwa na mtu mmoja mbunifu kutoka Ufaransa. Jules Rimet, aliyezaliwa Oktoba 14, 1873, Theuley, Mashariki mwa Ufaransa, na Mkatoliki alianzisha Red Star Sports Club 1897.

 Mfaransa huyo alihusika katikauzinduzi wa shirikisho la kusimamia kandanda ulimwenguni(FIFA) mwaka wa 1904. Lakini juhudi zake za kuanzisha jamii ya kandanda ya kimataifa zilitatizwa na vita vya kwanza vya dunia mwaka wa 1914

Baada ya vita hivyo kuisha, ambapo alikuwa mwanajeshi wa Ufaransa, Rimet alichaguliwa kama rais wa FFF(French Football Federation) mwaka wa 1919. Machi 1, 1921, Rimet alifanywa kuwa rais wa FIFA ambapo alilenga kuanzisha mashindano ya ulimwengu wote.

 Mipango yake ya Kombe la Dunia hata hivyo ilipata changamoto kubwa kutoka kwa vyama vidogo vya kandanda na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki(IOC) chini ya Pierre de Coubertin.

Tuzo la mashindano hayo lilipewa jina la raia huyo wa Ufaransa, 1930, ambapo mataifa kadhaa ya Amerika Kusini yalizuru Uruguay kwa mashindano hayo.

Baada ya kufaulu kwa mashindano hayo, Rimet alisalia rais wa muda mrefu zaidi wa FIFA-kwa miaka 33. Alianzisha mashindano hayo na wanachama 12, lakini alipoondoka, yalikuwa na wanachama 85. Aliaga dunia 1956, akiwa na miaka 83.
Kombe la Dunia la Kwanza

No comments:

Post a Comment