Hizi Hapa Timu 6 ambazo zinawachezaji wengi kwenye Michuano ya Kombe la Dunia - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 9 June 2018

Hizi Hapa Timu 6 ambazo zinawachezaji wengi kwenye Michuano ya Kombe la DuniaKUELEKEA KOMBE LA DUNIA, URUSI 2018: Ikiwa zimebaki siku 6 kuanza kwa Michuano hiyo. Je, unafahamu ni Klabu gani ambazo wachezaji wake wengi wameenda kwenye michuano hiyo?

Mara nyingi baada ya msimu kuisha kukiwa na michuano ya kimataifa klabu nyingi zinaanza kujiandaa kwa ajili ya msimu unaofuata(Pre-season) bila wachezaji wao kadhaa
-
Kwa mfano Liverpool itakuwa bila wachezaji wake 8 wakati wa kujiandaa kwa msimu ujao wakati klabu ya Juventus itakuwa bila wachezaji wake 11 japokuwa timu ya taifa ya Italy haijafuzu katika michuano hiyo
-
Vilabu 6 ambavyo vinawachezaji wengi kwenye Michuano ya Kombe la Dunia msimu huu ni;
1. Manchester City ya Uingereza - Wachezaji 16
2. Real Madrid ya Uhispania - Wachezaji 15
3. Barcelona ya Uhispania - Wachezaji 14
4. Chelsea ya Uingereza - Wachezaji 14
5. Paris Saint-Germain ya Ufaransa - Wachezaji 12
6. Tottenham ya Uingereza - Wachezaji 12

Je, unadhani wachezaji kutoka katika ligi ya nchi gani watafanya vizuri zaidi kwenye michuano hiyo?

No comments:

Post a Comment