Hiki Ndicho Alichokiona Mr Blue Kutoka kwa Daimond na Alikiba - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 23 June 2018

Hiki Ndicho Alichokiona Mr Blue Kutoka kwa Daimond na Alikiba

Staa wa muziki wa Hip Hop Bongo, Kherry Sameer ‘Mr Blue’, ambaye yupo kwenye gemu tangu mwaka 1999, akiwa amefanikiwa kufanya albamu mbili, Mr Blue na Yote Kheri, amefunguka kuwa wanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Salehe Kiba ‘Alikiba’, wana vitu vya ziada vinavyowafanya wazidi kufanikiwa.Akichonga na Mikito Nusunusu, Mr Blue alisema kwamba wanamuziki wengi chipukizi hutamani kuwa kama wawili hao bila kufahamu mbali na kufanya muziki wanajituma, wana nidhamu na wana malengo ya kufika mbali.“Unajua wengi hutamani kuwa kama fulani kwenye muziki hasa watu wanaofanya vizuri zaidi kwa sasa kama Diamond na Kiba, lakini bila kufahamu kwamba ili ufanikiwe ni lazima uwe na vitu vya ziada mbali na kuimba kawaida.“Kwa ushauri wangu, wanamuziki chipukizi waangalie ni vitu gani vya ziada wanavyo wanamuziki wanaotamani kuwa kama wao wavifuate na wataweza kufika kule wanako kuhitaji,” alisema Mr Blue.

No comments:

Post a Comment