Hali ilivyo kwa Hamisa Mobetto Baada ya Kusikia Baba Mtoto wake Majizzo Anamuoa Lulu Michael - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 25 June 2018

Hali ilivyo kwa Hamisa Mobetto Baada ya Kusikia Baba Mtoto wake Majizzo Anamuoa Lulu MichaelMsanii wa Bongo movie na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto ameweka wazi kuwa hana kinyongo na kutoa baraka zote kwa ajili ya ndoa ya Lulu na Majizzo.


Hamisa ambaye  amewahi kuwa kwenye Mahusiano na Majizzo siku za nyuma na  kuzaa naye mtoto mmoja ameweka wazi kuwa hivi sasa hana matatizo na Majizzo wala Lulu hivyo kwake ni Poa tu wakifunga ndoa.


Kwenye mahojiano na Risasi Jumamosi, Mobeto alisema kuwa hana kinyongo na Lulu kama ambavyo watu wanasema kwa kuwa mapenzi yake na Majizzo yalishakwisha siku nyingi.


"Mimi na huyo anayetaka kumuoa tulishamalizana, hivyo hakuna tena hata chembe ya mapenzi zaidi ya uhusiano wetu wa kulea mtoto.


"Kwa maana hiyo sina shida kusikia Lulu anaolewa na siku ya sherehe nikipewa kadi nitakwenda“.


Tangu Lulu atoke jela Kumekuwa na tetesi nyingi kuwa yeye pamoja na mpenzi wake Majizzo wanategemea kufunga ndoa hivi karibuni

No comments:

Post a Comment