Hakuna Mwanamke Wa Kunipindua Kwa Dogo Janja- Uwoya - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 18 June 2018

Hakuna Mwanamke Wa Kunipindua Kwa Dogo Janja- UwoyaMuigizaji wa Bongo movie mrembo Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa bado hajaona mwanamke ambaye anaweza kimpindua kwa mume wake staa wa Bongo fleva Abdul Chende ‘Dogo Janja’.

Uwoya ameweka wazi kuwa yeye ni mwanamke anayejiamini sana na anaamini kuwa mume wake anampenda na anajua kuwa hakuna mwanamke anayeweza kuingilia penzi lao.

Irene Uwoya amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Global Publishers ambapo amesema alipoamua kuingia kwenye ndoa na mwanamuz­iki huyo alijua wazi ‘nyakun­yaku’ wapo, la­kini kikubwa anajiamini.

Mimi sio mwan­amke wa kufuatana na mume nyuma kwa sababu najiamiani kuliko na ninajua wazi hakuna ambaye anaweza kunin­yakulia mume wan­gu. Najiamini kila idara mimi sina wasiwasi wowote”.

Uwoya amesisitiza kuwa hata mume wake aende wapi na aone mwanamke gani hawezi kumuacha yeye maaana anajiamini na anaamini kuwa amekamilika idara zote.

No comments:

Post a Comment