HABARI NJEMA, SALAH APONA MAJERAHA YAKE ASILIMIA 100, ATAKIPIGA DHIDI YA URUGUAY IJUMAA - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 14 June 2018

HABARI NJEMA, SALAH APONA MAJERAHA YAKE ASILIMIA 100, ATAKIPIGA DHIDI YA URUGUAY IJUMAA


Ripoti kutoka Urusi zinaeleza kuwa nyota wa Liverpool na timu ya taifa ya Misiri, Mohamed Salah ameshapona majeraha yake.

Mchezaji huyo anapewa nafasi kubwa ya kukiongoza kikosi cha Misri Ijumaa ya wiki ijayo dhidi ya Uruguay ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa taifa hilo katika michuano ya Kombe la Dunia inayoanza leo.

Salah aliumia katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa kuchezewa rafu na nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos kisha kusababisha kuondolewa nje ya Uwanja.

Kupona kwa Salah kumeongeza matumaini kwa Waafrika na Wamisri kwa ujumla kwenye safu ya ushambuliaji wa timu hiyo kutokana na mchango wake mkubwa Uwanjani.

No comments:

Post a Comment