GRIEZMANN ASEMA TAYARI AMESHAAMUA WAPI ANAELEKEA MSIMU UJAO - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 13 June 2018

GRIEZMANN ASEMA TAYARI AMESHAAMUA WAPI ANAELEKEA MSIMU UJAO


Straika hatari wa Atletico de Madrid, Antoine Griezmann, amesema kuwa tayari ameshafikia mwafaka wa wapi atakuwa msimu ujao lakini akishindwa kupataja.

Kwa mujibu wa Sky Sports, wameeleza kuwa mchezaji amekuwa akiwindwa kwa udi na uvumba na klabu za Manchester United na FC. Barcelona ambao wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili.

Tangu msimu wa ligi kuu Spain ukiwa haujamalizika kumekuwa na taarifa nyingi za nyota huyo tegemo wa Atletico kuhusishwa kujiunga na Barcelona.

"Ni kweli tayari nimeshanya maamuzi yangu, lakini si muda mwafaka wa kueleza nitaenda wapi," alisema.

No comments:

Post a Comment