DK.SHEINAZUNGUMZA NA VYAMA VYA UPINZANI LEO. - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 9 June 2018

DK.SHEINAZUNGUMZA NA VYAMA VYA UPINZANI LEO.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Vyama vya Upinzani katika mkutano wa ushauriano uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar(wa nne kushoto) Mwenyekiti wa CUF Taifa Mhe.Ibrahim Haruna Lipumba,[Picha na Ikulu.] 09/6/2018.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania Mhe.Magalie John P.Shibuda alipokuwa akitoa mchango wake katika Mkutano wa kushauriana na Vyama vya Upinzani pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) uliofanyika leo  katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 09/6/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Vyama vya Upinzani katika mkutano wa ushauriano uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar (wa nne kushoto) Mwenyekiti wa CUF Taifa Mhe.Ibrahim Haruna Lipumba, [Picha na Ikulu.] 09/6/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Vyama vya Upinzani baada ya  mkutano wa pamoja wa ushauriano uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na  Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania Mhe.Magalie John P.Shibuda   wakati wa  Mkutano wa kushauriana na Vyama vya Upinzani  uliofanyika leo  katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 09/6/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na   Mwenyekiti wa CUF Taifa Mhe.Ibrahim Haruna Lipumba,  wakati wa  Mkutano wa kushauriana na Vyama vya Upinzani  uliofanyika leo  katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 09/6/2018.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amekutana na viongozi wa vyama mbali mbali vya siasa kwa ajili ya kushauriana namna bora zaidi ya kuwapata wajumbe wawili watakaoteuliwa katika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutoka vyama vya upinzani.

Dk. Shein alikutana na viongozi hao leo huko Ikulu Mjini Zanzibar ambapo viongozi wa vyama 17 vya siasa walihudhuria wakiwemo Wenyeviti na viongozi wengine wa ngazi za juu wa vyama hivyo vya siasa ambapo hatua hiyo imekuja kwa ajili ya kutekeleza maelekezo ya  Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 katika kifungu chake cha 119 (1) c, kuhusiana na kuwapata wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (NEC).

Mkutano huo unafanyika baada ya Tume ya uchaguzi kumaliza muda wake chini ya Mwenyekiti wake Jecha Salim Jecha ambapo Tume hiyo ilifanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano kilichoanzia tarehe 30 April, 2013 mpaka tarehe 29 April, 2018 ambapo Wajumbe wake walifikia ukomo.

Kwa mujibu wa Rais Dk. Shein alieleza kuwa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 katika kifungu chake cha 119 (1) c, kimeweza kutoa maelekezo mazuri ambayo ndio njia moja wapo iliyokutanisha na viongozi hao wa vyama vya siasa hivi leo.

Dk. Shein alieleza kuwa katika kifungu hicho hicho cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu 119 (1) c, kinaeleza kuwa Wajumbe wawili watateuliwa na Rais kwa mapendekezo ya Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi au iwapo hakuna kiongozi wa upinzani basi kwa kushauriana na vyama vya siasa.

Hivyo, kwa maelezo ya Dk. Shein ameona haja ya kuwaita viongozi hao wa vyama vya siasa ili kushauriana nao juu ya nafasi hizo kutokana na hivi sasa kutokuwepo kwa kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

Dk. Shein alitumia fursa hiyo kulipongeza Baraza la Wawakilishi kwa kuweka mbadala katika kifungu hicho cha 119 (1) c, ambacho kimeweza kusaidia namna ya kuwapata wajumbe hao wawili kutoka vyama hivyo vya siasa.

Aidha, Dk. Shein aliwaeleza viongozi hao kuwa mara baada ya kumaliza taratibu za kuwapata viongozi hao kutoka vyama hivyo vya siasa atayateua majina hayo kupitia Tume mpya ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) inayotarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alisema kuwa nia yake ya kufanya hivyo ni kujenga Zanzibar kwa umoja na mshikamano na kuahidi kuwa hatobeza mawazo ya vyama vya siasa vya upinzani na kuahidi kutenda haki katika kuchagua viongozi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar walio wazuri.

Rais Dk. Sheinalieleza kuwa hatua hiyo ndio njia pekee itakayosaidia zaidi kuimarisha uongozi wa demokrasia hapa nchini huku akitumia fursa hiyo kuyapongeza mawazo ya viongozi hao wa vyama vya siasa waliyoyatoa katika kikao chao hicho.

Nao viongozi hao waliohudhuria katika kikao hicho waliupongeza uwamuzi wa Rais Dk. Shein wa kuwaita kwa lengo la kushauriana nao pamoja na kueleza kuwa kitendo hicho kinaonesha wazi kuwa kiongozi huyo amebobea katika demokrasia na utawala bora.

Viongozi hao walitoa shukurani kwa Rais Dk. Shein kwa kuvishirikisha vyama hivyo vya siasa na kupongeza kwa jinsi anavyoongoza nchi kwa hekima na busara na kuwa mvumilivu hatua ambayo imeipelekea Zanzibar kuwa ni nchi yenye amani,utulivu na kuweza kupiga hatua kubwa na kumfanya kila mmoja kupenda kuja kuishi.


Aidha, viongozi hao walimpongeza Rais Dk. Shein kwa ujuzi, hulka, silka ambavyo vyote hivyo ni vipaji vyake alivyopewa na MwenyeziMungu jambo ambalo kama wao viongozi wa siasa wamekuwa wakifarajika kwa tabia hiyo ya Rais Dk. Shein kutokana na uongozi wake mahiri.
Ramadhan Othman Abdalla

No comments:

Post a Comment