Diego Maradona azushiwa kifo baada ya bao la pili la Marcos Rojo dhidi ya Nigeria ‘Mimi mzima’ - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 27 June 2018

Diego Maradona azushiwa kifo baada ya bao la pili la Marcos Rojo dhidi ya Nigeria ‘Mimi mzima’

Gwiji wa soka nchini Argentina, Diego Maradona amethibitisha kuwa yupo bugheri wa afya baada ya kuzua taharuki juu ya afya yake na kuzushiwa kufa baada ya timu yake ya taifa kupata bao la pili dhidi ya Nigeria kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Urusi.
Maradona amesema kuwa alikunywa mvinyo mweupe ‘white wine’ kabla ya kuingia kushuhudia mechi hiyo hii ni mara baada ya kuzushiwa kufariki baada ya ushindi wao dhidi ya Nigeria.
Nguli huyo wa soka amewatupia lawama waliyo sambaza habari za uongo juu ya kifo chake kupitia mtandao wa WhatsApp huku sehemu ya ripoti hiyo ikielezwa kuwa chanzo cha kifo nikutokana na la moyo.
Baada ya kuonana na daktari huko Saint Petersburg Urusi ameeleza kuwa aliumia shingo wakati wa mchezo huo huku akikiri kunywa mvinyo kabla ya mechi na hata kushauriwa kuondoka kiwanjani hapo baada ya dakika 45 za kwanza zitakapo malizika swala ambalo hakutilia maanani.

No comments:

Post a Comment