DIAMOND PLATNUMZ ANUSURIKA KIFO KWA AJALI - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 23 June 2018

DIAMOND PLATNUMZ ANUSURIKA KIFO KWA AJALI


Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amenusurika katika ajali ya gari nchini Marekani ambapo upo kwa ajili ya tour ya albamu yake ‘A Boy From Tandale’

Muimbaji huyo amepata ajali hiyo wakati akitokea kwenye shoo.

Kupitia mtandao wa Instagram ameandika;

Dah Tumepata ajali na kunusurika kufa usiku wa leo wakati tunatoka kwenye show….ila Mwenyez Mungu ametupa nafasi nyingine tena ya kuishi na kuendelea kushikana mkono na vijana wenzangu mtaani kwa pamoja tuziokoe familia zetu duni.

Diamond ni ndiye mwanzilishi na mmiliki wa label ya WCB ambayo inasimamia wasanii kama Harmonize, Rayvanny, Rich Mavoko, Queen Darleen, Lava Lava na Mbosso.

Msanii Diamond Platnumz Amefunguka kuwa amenusurika Kifo Baada ya kupata ajali wakati akitoka katika show huko Huko Califonia Ncchini Marekani Kupitia kwenye Instagram yake Diamond Alikuwa na washkaji mbali mbali akiwemo Dj Wake Rommy Jons So wakati gari inaendelea kwenda wakapata ajali.

No comments:

Post a Comment