BUNDI AIBUKA TIMU YA TAIFA YA ARGENTINA, WACHEZAJI HAWAMTAKI TENA KOCHA - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 25 June 2018

BUNDI AIBUKA TIMU YA TAIFA YA ARGENTINA, WACHEZAJI HAWAMTAKI TENA KOCHA


Msala mkubwa umeibuka katika timu ya taifa ya Argentina kufuatia kipigo ilichokipata dhidi ya Croatia cha mabao 3-0, unaambiwa wachezaji hawamtaki Kocha wao Jorge Sampaoli.

Taarifa zilizopo hivi sasa zinaeleza kuwa nyota wa kikosi hicho wamegoma kupangiwa kikosi na Sampaoli baada ya kuoboronga mechi dhidi ya Croatia na kusababisha majonzi makubwa kwa wadau na mashabiki wa taifa hilo.

Awali kabla ya uteuzi wa kikosi kilichopaswa kucheza dhidi ya Croatia, wachezaji wa Argentina wakiongozwa na Nahodha wake, Lionel Messi walishauri kuwa na safu nzito ya mabeki lakini Sampaoli akapuuzia.

Kutokana na Sampaoli kukipanga kikosi hicho kwa aina anayotaka, ikiwa ni pamoja na kuweka mabeki watatu badala ya wanne kama walivyotaka wachezaji wameamua kumsusia kocha huyo asipange tena kikosi.

Inaelezwa kuwa wachezaji walifikia hatua ya kuitisha kikao na Rais wa Shirikisho la Soka Argentina, Claudio Tapia, wakishinikiza Kocha wao aondoshwe haraka ili mambo yaende sawia ndani ya kikosi hicho.

Kikao hicho cha dharura kilichoongozwa na Javier Mascherano kiliwakutanisha wachezaji na Rais kwenye Hotel ambayo wamefikia nchini Urusi na kujadili juu ya hatma ya Sampaoli ambaye wapmependekeza aondolewe.

Hata hivyo suala hilo limeshindwa kufanikiwa kirahisi japo wachezaji watakipiga na Nigeria katika mchezo ujao huku wakiwa hawatambui uwepo wa Sampaoli kama Kocha wao Mkuu.

No comments:

Post a Comment