BREAKING NEWS:DR.SHEIN AFANYA UTEUZI. - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 20 June 2018

BREAKING NEWS:DR.SHEIN AFANYA UTEUZI.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Kifungu 119 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).

Kwa mjibu wa taarifa iliyosainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, ilieleza kuwa Katika uteuzi huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amemteua Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Aidha, amewateua Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar akiwemo Mabruki Jabu Makame, Feteh Saad Mgeni, Makame Juma Pandu,Dk. Kombo Khamis Hassan, Jaji Khamis Ramadhan Abdalla na Jokha Khamis Makame.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 20 Juni 2018 ambapo Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi wanatarajiwa kuapishwa siku ya Ijumaa tarehe 22 Juni 2018 saa 4 za asubuhi Ikulu Mjini Zanzibar.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

No comments:

Post a Comment