BREAKING NEWS: SHABIKI AUA KWA RISASI, AJERUHI WANNE AKISHANGILIA USHINDI WA SWEDEN - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 19 June 2018

BREAKING NEWS: SHABIKI AUA KWA RISASI, AJERUHI WANNE AKISHANGILIA USHINDI WA SWEDEN


Mtu mmoja amefyatua risasi na kuua mtu mmoja huku ikielezwa amewajeruhi watu wengine wanne wakati akisherekea ushindi wa Sweden katika Kombe la Dunia.


Sweden iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi Korea Kusini. Na shabiki huyo katikati ya mji wa Malmo nchini Sweden, alifyatua risasi hovyo na kusababisha kifo hicho. 

Baadhi ya watu walieleza kwamba mtu huyo alikuwa amelewa na alifyatua risasi ili kuonyesha furaha yake baada ya ushindi huo wa Sweden wakati timu kadhaa maarufu katika soka duniani kama Ujerumani, Brazil na Argentina hazikuwa zimepata ushindi.

Haijafahamika kama polisi wamemkamata mhusika kwani baada ya tukio hilo kulikuwa na taharuki na watu wakikimbia hovyo.

No comments:

Post a Comment