Babu Tale Afunguka Ajali Aliyoipata Daimond Akiwa Marekani - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 25 June 2018

Babu Tale Afunguka Ajali Aliyoipata Daimond Akiwa Marekani

Moja ya Mameneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka kuhusu ajali aliyokumbana nayo muimbaji huyo akiwa nchini Marekani.

Babu Tale akizungumza na JJ wa Jembe Fm amesema kuwa ajali hiyo imetokana na dereva aliyekuwa nyuma kushinda kuzingatia taa.

“Nadhani ni dereva wa lile gari lingine hakuwa amezingatia taa, kwa hiyo alipita wakati gari ya kina Diamond linapita ndio akawagonga,” amesema Babu Tale.

Utakumbuka June 23, 2018 Diamond Platnumz ndiye aliyeweka wazi kunusurika katika ajali hiyo ya gari akiwa nchini Marekani ambapo upo kwa ajili ya tour ya albamu yake ‘A Boy From Tandale’, hata hivyo hakuna majeruhi yeyote aliyeripotiwa.

No comments:

Post a Comment