BAADA YA KUPATA KIPIGO, KOCHA ARGENTINA AIBUKA NA KUZUNGUMZA MAZITO - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 23 June 2018

BAADA YA KUPATA KIPIGO, KOCHA ARGENTINA AIBUKA NA KUZUNGUMZA MAZITO


Kocha wa timu ya taifa ya Argentina, Jorge Sampaoli, ameamua kufunguka juu ya kipigo alichokipata dhidi ya Croatia cha mabao 3-0.

Mchezo huo wa michuano ya Kombe la Dunia ulimalizika kwa Waargentina kukatishwa tamaa na Sampaoli kama anaweza kuivusha timu hiyo kuelekea hatua inayofuata.

Kocha huyo ameibuka na kueleza kuwa lawama zote zilistahili kuelekezwa kwake kutokana na kiwango cha timu yake kilivyokuwa.

Sampaoli ameona isiwe tabu kutokana na lawama nyingi zikielekezwa kwake pamoja na Lionel Messi ambaye anategemewa zaidi na mashabiki wa timu hiyo.

Kipigo hicho kimeifanya Argentina iendelee kusalia na alama moja pekee baada ya mchezo wa kwanza dhidi ya Iceland kwenda sare ya bao 1-1.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Lionel Messi alionekana akikosa furaha kutokana na asilimia kubwa ya mashabiki wa Argentina kuwa na imani naye kuwa anaweza akwasaidia kuifikisha timu 16 bora.

No comments:

Post a Comment