AS ROMA yashindwa kujizuia kuhusu Nigeria - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 27 June 2018

AS ROMA yashindwa kujizuia kuhusu Nigeria


Klabu ya AS ROMA inayoshiriki ligi kuu ya nchini Italia imeonesha heshima yao na pongezi kwa timu ya taifa ya Nigeria baada ya kumalizika kwa mchezo wa mzunguko wa tatu, hatua ya makundi ya kombe la Dunia  nchini  Urusi .

Klabu hiyo imeandika ujumbe huo wa pongezi  kupitia mtandao wa Twitter ambao ulisomeka;

“ Ni masikitiko kuwa safari imeisha kwa 'Super Eagle's na mashabiki wao machachari, mlikuwa na jezi nzuri zaidi ambazo zilipambwa na hali ya upambanaji na kujivunia kwenu . Tumetengeneza marafiki wapya ambao wengine watabaki na wengine wataondoka, lakini tunatumani  siku moja tutaonana Roma au tutatembelea Lagos. #StillForzaSuperEagles “. Ulieleza ujumbe huo.

Nigeria imeondolewa katika michuano ya kombe la Dunia baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa Argentina ambayo ilikuwa inahitaji alama tatu ili iweze kufuzu hatua ya 16 bora. Goli lililouwa matumaini ya Nigeria kufuzu hatua inayofuata lilifungwa na mlinzi Marcos Rojo baada ya kuunganisha 'frikiki' ya haraka muda mfupi kabla ya kumalizika kwa mchezo huo.

Gumzo kubwa la mchezo huo ni Penalti ya pili ya Nigeria iliyokataliwa na teknolojia ya usaidizi wa video kwa mwamuzi (VAR) ambayo wengi wa wadau wanaijadili kuwa ilikuwa ni sahihi na wengine wanasema haikuwa sahihi na ilikuwa sawa kukataliwa.

Sasa Argentina itakutana na Ufaransa katika hatua ya 16 bora na katika mchezo huo pia gwiji wa zamani wa Argentina, Diego Maradona alikimbizwa Hospitali baada ya kuzidiwa kwa furaha ya ushindi muda mfupi baada ya timu yake kufunga bao la pili na mchezo kumalizika.

Matumaini ya Waafrika yamebakia kwa Simba wa Teranga ( Senegal ) ambayo ina alama 4 mpaka sasa na mchezo wa mwisho wa hatua hii ya makundi itacheza Alhamisi dhidi ya Colombia ambapo Senegal inahitaji ushindi au sare ili iweze kufuzu hatua ya 16 bora.

No comments:

Post a Comment