Arsenal mbioni kumchukua Lucas Torreira - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 13 June 2018

Arsenal mbioni kumchukua Lucas Torreira


Klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza ipo kwenye mazungumzo na kiungo wa Uruguay, Lucas Torreira anaekipiga Sampdoria inayoshiriki ligi ya Serie A ili kuona kama wataweza kunasa saini yake.

Kiungo huyo wakati mwenye umri wa miaka 22 anapewa nafasi kubwa ndani ya the Gunners huku ikiripotiwa kutengewa bajeti ya pauni milioni 26.

Mpaka sasa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa kwa Torreira ambaye yupo nchini Urusi kwenye michuano ya kombe la Dunia. Mpaka sasa The Gunners imemsajili beki wa Uswis, Stephan Lichtsteiner kwa uhamisho huru akitokea Juventus.

No comments:

Post a Comment