Aliyegongelewa Misumari Miwili Kichwani na Bosi Wake Amefariki - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 22 June 2018

Aliyegongelewa Misumari Miwili Kichwani na Bosi Wake Amefariki

Mwanaume aliyepigiliwa misumari miwili na Bosi wake kichwani nchini Kenya amefariki katika hospitali ya taifa ya Kenyatta.

Robert Muchangi amefariki leo June 21, 2018 katika hospitali ya taifa ya Kenyatta alipokuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kukumbwa na kisanga hicho mjini Meru.

Ikumbukwe kuwa Muchangi alipigiliwa misumari miwili kichwani kwake na Bosi wake baada ya kwenda kumdai fedha walizokubaliana baada ya kumjengea nyumba Bosi wake huyo.

Aidha Muchangi ameacha bili ya zaidi ya Shilingi Milioni 6 za Kitanzania katika hospitali hiyo ambazo ndugu zake wanatakiwa wazilipe.

Kwa upande mwingine ndugu zake Muchangi wamelilalamikia jeshi la Polisi nchini humo kwa kukaa kimya juu ya tukio hilo.

No comments:

Post a Comment