Adakwa kwa kuuza sambusa za Paka - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 25 June 2018

Adakwa kwa kuuza sambusa za Paka


Maafisa wa Polisi nchini Kenya wanamshikilia mwanaume mmoja anayejulikana kama James Mukangi, kwa kuwauzia watu sambusa zinazotengenezwa kwa nyama ya paka.

Mukangi amekamatwa Jumapili ambapo inadaiwa amekutwa akimchuna ngozi paka, huku akidaiwa kuwauzia wauzaji wa sambusa nyama hiyo, na pia wenye migahawa, Gazeti la Star limesema mwenyewe amekiri kupika sambusa kwa kutumia nyama hiyo.

Taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari nchini humo, zinasema Mukangi amekiri kuuza nyama ya paka zaidi ya elfu moja mjini humo tangu mwaka 2012.

Mukangi amewaambia wanahabari kwamba ameanza biashara hiyo baada ya kuona upungufu wa nyama sokoni, "Huwa nawaambia wateja wangu kwamba huwa naipata nyama hii kutoka Gioto (jaa la kutupa taka), lakini huwa hawajui kwamba ni nyama ya paka," amenukuliwa na gazeti la Nation.

Aidha Mukagi ameongeza kuwa huwa anauza pia ngozi za paka na kwamba kwa kila paka hujipatia takriban Shilingi 500 sawa na (Dola 5 za Marekani).

No comments:

Post a Comment