14 Wafariki kwa Ajali ya Roli na Daladala Mkuranga - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 25 June 2018

14 Wafariki kwa Ajali ya Roli na Daladala Mkuranga

Watu 14 wamefariki dunia na wengine 4 wamejeruhiwa baada ya Gari dogo aina ya Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na Lori la Mchanga lenye namba za usajili T 439 DCC  katika kijiji cha Dundani wilayani Mkuranga.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Dkt.Steven Mwandambo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na zoezi linaloendelea kwa sasa ni kuwanasua baadhi ya majeruhi walionasa katika magari hayo.

No comments:

Post a Comment