Steve Nyerere ataka wasanii kumiliki bima, ”tutakuwa watu wa kuomba msaada” - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 1 May 2018

Steve Nyerere ataka wasanii kumiliki bima, ”tutakuwa watu wa kuomba msaada”

Msanii wa filamu Tanzania, Steve Nyerere ametoa ushauri mkubwa sana kwa wasanii ambao hawana bima za afya kuhakikisha wanamiliki bima hizo kwa ajili yao na familia zao.
Steve amesema hayo hayo akidai kuwa ifike kipindi wasanii wamiliki bima zao ili wasiwe watu wa kuomba msaada pindi wanapokabiliwa na matatizo ya kiafya na amedai kuwa Bima ya afya ni mkombozi wao.
Amezungumza hayo kufuatia kitendo cha Mzee Majuto ambaye siku chache zilizopita aliomba msaada wa kuchangiwa pesa kwa ajili ya matibabu nchini India.
”Wasanii wenzangu bima ya afya ni kitu muhimu kwako na kwa familia yako, Bima ya Afya ni mwokozi kwetu. Sidhani kama miaka nenda rudi tutakuwa watu wa kuomba msaada ,tujiulize tunafanya mapart, tunakunywa na kusaza ,tunajinadi kwenye mitandao nguo zetu kuanzia milioni 3 mpaka 4 tukiulizwa umejipangaje kwa kesho amna kitu, ni muda wa kuamka sasa ,naamini majukumu hayakimbiliki bali tunayakabili” amesisitiza Steve Nyererere
Steve Nyerere hakuishia hapo alikwenda mbali zaidi na kuwataka wasanii wajifunze kupitia kwa Mzee Majuto kuwa kuna ulazima mkubwa wao kuwa na bima ya afya.

No comments:

Post a Comment