Polisi abakwa alipokwenda kumkamata mbakaji - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 1 May 2018

Polisi abakwa alipokwenda kumkamata mbakaji

Askari Polisi mmoja wa kike huko Yorkshire Kusini, nchini England ameripoti kubakwa na mwanaume ambaye alikwenda kumkamata akiwa na askari mwingine kwa makosa ya jaribio la kubaka.
Mwanaume huyo alikuwa akihisiwa kufanya vitendo hivyo vya kujaribu kubaka watoto wa kike na ndipo askari huyo alipokwenda na mwenzie kumkamata ili afikishwe polisi.
Katika harakati hizo za kumkamata mwanaume huyo anadaiwa kuwapiga na kuwajeruhi kisha kumbaka huyo askari mmoja.
Inaelezwa kuwa mwanamume huyo tayari amekwisha kamatwa na amefungulia mashtaka ya kujaribu kubaka, shambulio, unyanyasaji wa kijinsia na uharibifu wa makosa ya jinai.

No comments:

Post a Comment