NJEMBA AMUUWA MPENZI WAKE KWA KUMNYONGA SHINGO - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 1 May 2018

NJEMBA AMUUWA MPENZI WAKE KWA KUMNYONGA SHINGO

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia kijana aliyefahamika kwa jina la Nicholas Light (25) mkazi wa Mtaa wa Mahama, wilayani Ilemela akituhumiwa kumnyonga mpenzi wake Victoria Swai (26)baada ya kumkaba shingo hali iliyosababisha kukosa hewa na kupoteza uhai.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai tukio hilo limetokea katika jengo la Ekacliff Ofisi ya Kilimanjaro Avitaion ambapo baada ya polisi kufanya uchunguzi katika nyumba alipokuwa akiishi marehemu na mpenzi wake, walimkuta mtuhumiwa akiwa amejificha juu ya dari ya nyumba.

Jeshi limesema, chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi ambapo mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu mpenzi wake (marehemu) kuwa alikuwa akimsaliti kimapenzi.

Mwili wa marehemu Victoria umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi, pindi utakapokamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

No comments:

Post a Comment