LIGI YA MABINGWA ULAYA, MMOJA KUTINGA FAINALI LEO KATI YA MADRID VS BAYERN - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 1 May 2018

LIGI YA MABINGWA ULAYA, MMOJA KUTINGA FAINALI LEO KATI YA MADRID VS BAYERNLigi ya Mabingwa Barani Ulaya inaendelea leo katika mchezo wa marudiano kati ya Real Madrid watakaokuwa nyumbani kuikaribisha Bayern Munich.

Madrid watakuwa nyumbani Santiago Bernabeu wakiwa na faida na bao moja kufuatia ushindi wa 2-1 ugenini kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.

Mechi hiyo itakayoanza majira ya saa 3 na dakika 45 kwa saa za Afrika mashariki utatoa mshindi atakayetangulia kwenye hatua ya fainali ya mashindano hayo.

Mshindi wa pili atasubiriwa kesho ambapo majogoo wa Anfield, Liverpool watakuwa wageni dhidi ya AS Roma huko Italy.

No comments:

Post a Comment