ZFA YAMTUPIA LAWAMA NICHOLAS MUSONYE, YAMTAJA KUWAFANYIA FITINA ZA KUWAONDOA CECAFA - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 18 April 2018

ZFA YAMTUPIA LAWAMA NICHOLAS MUSONYE, YAMTAJA KUWAFANYIA FITINA ZA KUWAONDOA CECAFA


Baada ya kuondolewa katika mashindano ya CECAFA, Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), limemcharukia Katibu wa Mkuu wa Baraza hilo, Nicholas Musonye.

Musonye ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, ametuhumiwa kuifanyia njama za kuiondoa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Karume Boys, baada ya kubainika kuwa wachezaji 12 wamezidi umri.

Kwa mujibu wa Shirikisho hilo, limeeleza kuwa Musonye amekuwa hana maelewano mazuri na Zanzibar kuhusiana na mashindano hayo, hivyo ametumia kama mbinu ya kuwakomoa kwa kuwaondoa sababu ya kisingizio cha kuzidi umri wa wachezaji, uongozi ulieleza.

Kutokana na tukio hilo kutokea, uongozi wa ZFA umekemea kitendo hicho wakisema kuwa wameonewa ikiwa ni siku moja baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kusema itaingilia kati kufanya uchunguzi juu ya kuondolewa kwa kikosi cha Karume Boys.

Mbali na Karume Boys, Ethiopia nayo ilikumbana na rungu la kuondolewa sambamba na faini ya kiasi cha dola za kimarekani 15,000, kutokana na wachezaji kadhaa kuzidi umri stahiki.

No comments:

Post a Comment