Yanga yapangwa kundi D michuano ya kombe la Shirikisho Afrika - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 21 April 2018

Yanga yapangwa kundi D michuano ya kombe la Shirikisho Afrika

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limetangaza droo ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika huku wawakilishi wa Tanzania timu ya Yanga SC ikipangwa kundi D.

Droo hiyo iliyofanyika makao makuu ya CAF , Cairo nchini Misri Yanga SC  imepangwa kundi D na kuungana na timu za Rayon Sports (Rwanda), U.S.M Alger (Algeria) na Gor Mahia (Kenya) .

Yanga SC imetinga hatua ya makundi baada ya kuifunga timu ya Welayta Dicha ya nchini Ethiopia kwa jumla ya mabao 2 – 1.


No comments:

Post a Comment