Yanga SC kutua Dar kimya kimya - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 19 April 2018

Yanga SC kutua Dar kimya kimya


Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga wanatarajia kurejea majira ya saa 7:10 usiku wa leo kutoka Ethiopia walipokuwa wakicheza mchezo wao wa klabu bingwa Barani Afrika dhidi ya Welayta Dicha.

Picha ya pamoja na balozi wa Tanzania nchini Ethiopia mara baada ya chakula cha mchana Leo hii jijini Addis Ababa.
Kabla ya kurejea nchini kikosi cha Yanga SC kimepata nafasi ya kula chakula cha mchana nyumbani kwa balozi wa Tanzania jijini Addis Ababa.
Yanga SC inarejea nyumbani ikiwa na furaha ya kufanikiwa kusonga mbele hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kuisukumiza nje timu ya Welayta Dicha ya Ethiopia kwa jumla mabao 2 – 1.

No comments:

Post a Comment