Wengine watatu wanaodaiwa kutekwa Mtambwe wapatikana, wakamilisha idadi ya watu sita - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 15 April 2018

Wengine watatu wanaodaiwa kutekwa Mtambwe wapatikana, wakamilisha idadi ya watu sita

Image result for kutekwa
Watu watatu  wengine kati ya wale sita waliyodaiwa kutekwa na kuchukuliwa na watu wasiojuulikana wameokotwa saa 8 usiku wa kuamkia leo katika maeneo tofauti huku hali zao zikielezwa kuwa ni mbaya na hivi sasa wapo hospitali ya wete wakiendelea kupata matitabu.
Watatu hawa na wale waliosalia kati wa watatu walioachiwa hivi majuzi
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kiongozi wa wa jumuiya ya vijana CUF  Mtambwe ndg ; Mohd Khatib amesema vijana hao wameokotwa katika maeneo tofauti ambapo wawili kati yao waliokotwa Mzambarauni  na mmoja ameokotwa Likoni njia ya kuvukia kuelekea kojani.
” Mzambarauni  waliokotwa Thuwein Nassor Hemed pamoja na Khamis Abdalla Mattar na Likoni aliokotwa Khalid Khamis  Hassan” alisema Mohd
Nd Mohd amesema , kutokana na doria maalum waliyokua wakiifanya wananchi wa jimbo la Mtambwe ndio kulikofanikisha kuonekana kwa vijana hao ambapo amesema vijana wa doria walishitushwa kuiona gari isiyokua na nambari ikitembea hivyo kuitilia mashaka na walipoanza kuifatilia waliikosa kidogo lakini na baadae ndipo walipowaona watu hao wakiwa washatupwa.
Akizungumzia hali za watu hao amesema , bado afya zao si za kuridhisha kwa sababu hawawezi hata kuzungumza na miguu  imewavimba kiasa ambacho hawawezi hata kusimama.
Nae Saidi Nassor  Hemed ambae ni kaka wa Tuhuweini Nassor Hemed amesema hali sio nzuri kwani hadi muda huu wapo katika hospitali na watu wao hawawezi kuzngumza ” hali zao ni mbaya , hawawezi kuzungumza , wamekonda sana lakini katika migongo yao wanamakovu mengi ya kupigwa na kitu kama waya hivi ” alisema Said.
Aidha amesema kuwa watu hao wanaharisha damu na wanakwenda haja ndogo yenye kutoka sambamba na damu.
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini Pemba Haji Khamis Haji amethitibisha kupatika kwa vijana hao ambapo amesema bado hawajapata maelezo ya vijana hao kutokana na kuwa katika harakati za kimatibabu.
” tutakapo tuzungumza nao ndio tutajua nini kinaendelea lakni mpaka sasa wapo hospitali wanaendelea na matibabu ” alisema kamanda huyo

No comments:

Post a Comment