Waziri ampa shavu Ali Kiba - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 30 April 2018

Waziri ampa shavu Ali Kiba


Msanii wa muziki wa bongo fleva Alikiba ambaye jana April 30, 2018 alifanya sherehe ya kumkaribisha mkewe, Amina ambaye ni raia wa Kenya jana amepewa shavu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla kwenda katika mbuga zozote zile kwa gharama yake.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla alisema hayo jana na kuwapa nafasi hiyo maharusi hao Alikiba na mkewe pamoja na Abdukiba na mkewe kwenda kutembelea katika mbuga za wanyama za Tanzania.

"Nimeona Waziri wa Utalii siwezi kuwepo hapa bila kutoa zawadi kwa maharusi wetu kwenda kupumzika siku yoyote mkitaka kesho, mkitaka baada ya wiki moja au hata baada ya mwezi mtachagua sehemu ya kwenda kwa gharama zangu, sehemu yoyote ndani ya nchi hapa wewe utanipigia tu tutapanga kwa ajili yako, usafiri wa juu na chini kwenda na kurudi ili uende ukapumzike na bi harusi" alisema Kigwangalla

No comments:

Post a Comment