Waliokataa Wito wa Makonda Kufikishwa kwa Kamanda Mambosasa - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 21 April 2018

Waliokataa Wito wa Makonda Kufikishwa kwa Kamanda Mambosasa

Waliokataa Wito wa Makonda Kufikishwa kwa Kamanda Mambosasa
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amewaonya wanaume waliokataa wito wa kuitwa kwao kuhusiana na malezi ya mtoto kufanya hivyo mara moja, la sivyo anapeleka majina yao kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam Lazaro Mambosasa, ili wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.


Makonda ametoa kauli hiyo alipokuwa akiongea na kina mama ambao wametelekezwa kulea watoto na baba wa watoto waliozaa nao, na kusema kwamba muda wa kubembelezana umkwisha, kinachofuata ni kuhakikisha wanaume hao wanakamatwa na jeshi la polisi ili kuwawajibisha.

“Kwa mwanaume yeyote ambaye amepigiwa simu, amepelekewa barua halafu amakaidi wito, kuanzia Jumatatu ninawakamata wanaume waliokimbia majukumu yao, ambao hawajafika, siku ya Jumapili majina yao wote yataenda kwa Mambosasa, na mtaanza kushughulikiwa, siwezi kuongoza mkoa unaendelea kuwa na idadi ya watoto ombaomba wakati baba zao wapo”, amesema Paul Makonda.

Pia Paul Makonda amesema hafanyi hivyo kwa ajili ya kuwatetea wasaidizi wa kazi (house girl) aliyelala na baba mwenye nyumba au katibu muhtasi (secretary) aliyetembea na bosi, bali anafanya hivyo kwa ajili ya kuwasaidia na kuwalinda watoto ambao hawana hatia.

“Na simtetei housegirl aliyelala na baba mwenye nyumba akavunja ndoa, simtetei secretary aliyelala na bosi wake akafanya mpaka akapanda cheo, ninayemtetea ni mtoto aliyezaliwa bila kuchagua kuzaliwa hapo”, amesema Paul Makonda. 

No comments:

Post a Comment