VIDEO:Kuhusu video chafu: Diamond na Nandy waomba radhi, Wadai enzi zimebadilika wamejifunza - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 19 April 2018

VIDEO:Kuhusu video chafu: Diamond na Nandy waomba radhi, Wadai enzi zimebadilika wamejifunza


Wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Nandy leo Aprili 19, 2018 wamejitokeza hadharani na kuwaomba radhi Watanzania kutokana na kusambaza video zao za faragha kwenye mitandao ya kijamii.
Diamond akiwa na Nandy mbele ya Waandishi wa Habari katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) amesema kuwa kwa sasa amejifunza sheria za makosa ya kimtandao ambapo amedai kuwa hatarudi tena kufanya hivyo.
Kuna vipande vya video (Clips) ambazo zimekuwepo na zinanihusu ambazo hazikuwa nzuri kiukweli. Pengine katika tamaduni za zamani tungeona kama barida tu! lakini sasa kwa kanuni hizi ambazo zimetengenezwa kutusaidia sisi na vijana wote ili baadae taifa lipate sifa nzuri kiujumla, basi tuziache na tufanye vitu vilivyokuwa vizuri na kwa mtu ambaye zilimkwaza pengine, tuvumiliane, tusameheane tu,“amesema Diamond Platnumz.
Nandy naye amesema ameukosea umma kwa video yake hivyo ameona hana budi kuomba radhi, ambapo ameendelea kusisitiza kuwa sio yeye aliyevujisha video hiyo na kwa sasa ameshajifunza sheria mpya za uhalifu au makosa ya mitandaoni (Cyber crime) na hata rudia tena.
Kiukweli nimejifunza vitu vingi sana, nimejifunza kuwa sio sahihi kuchukua clip ukiwa mtupu na kuipeleka mtandaoni, nilijutia kwa kipindi hicho kujichukua video kama ile na nimehuzunika sana kwa video hii kutoka nje  Nipo tayari kushirikiana na serikali kwa hili lililotokea kutoa elimu kwa jamii kiujumla wanafunzi. Unajua watu wengi wanafanya hivi vitu lakini hawajulikani. Naomba radhi kwa niaba ya watu waliofanya hiki kitendo na naomba radhi kwa mashabiki najua wengi wanachukulia labda kama kiki lakini haikuwa ridhaa yangu kitu kama hiki kitokee,”amesema Nandy.
Wiki iliyopita Diamond na Nandy waligonga vichwa vya habari nchini Tanzania baada ya video zao za faragha kusambaa mitandaoni.

No comments:

Post a Comment