Uteuzi alioufanya Rais Magufuli muda huu - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 20 April 2018

Uteuzi alioufanya Rais Magufuli muda huu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora.

Bw. Makungu anachukua nafasi ya Dkt. Thea Ntara ambaye amestaafu.

Uteuzi wa Bw. Makungu unaanzia tarehe 20 Aprili, 2018 na tarehe ya kuapishwa kwake itapangwa baadaye.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
20 Aprili, 2018

No comments:

Post a Comment