Usiyoyajua Kuhusu Kufikia Kileleni Wakati wa Tendo la Ndoa - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 21 April 2018

Usiyoyajua Kuhusu Kufikia Kileleni Wakati wa Tendo la Ndoa

Makala ya leo itasaidia kujibu maswali ninayoyapokea mara kwa mara kutoka kwa wasomaji wanaotaka kujua nini maana ya kufika kileleni au mshindo wakati wa tendo la ndoa?

Kufika kileleni au kufika mshindo kwa lugha ya kitabibu hujulikana kama ‘orgasm’ na kwa lugha ya Kiingereza huitwa ‘coming’ au ‘climaxing’.

Ni tukio linalohusisha usisimuliwaji wa kimwili na kiakili, makala hii itajikita katika aina ya kufika kileleni inayotokea wakati wenza wawili wanaposhiriki tendo la ndoa.

Kufika kileleni ni msisimko wa kipekee unaoleta hisia nzuri kwa wenza wawili wanaowajibika kikamilifu katika tendo la ndoa. Hisia hizi hutokea kwa wenza wote kama ishara ya kufikia kilele cha tendo.

Hisia hizo huambatana na mtiririko wa matukio kadhaa yanayohusisha mfumo wa fahamu (ubongo na mishipa ya neva), damu na moyo na maeneo mengineyo ikiwamo viungo vya uzazi.

Wenza wanapofika kileleni mapigo ya moyo hubadilika, hudunda kwa haraka na huku upumuaji ukiwa ni wa kasi na kuvuta pumzi kwa nguvu.

Kwa wanawake, hali hii huwa ni nzito na yakipekee, kufika kwao kileleni nakupata hisia nzuri huweza kuambatana na kujikunja ama kujikaza kwa misuli ya maeneo ya sehemu za siri, nyumba ya uzazi na kiunoni.

Mwanamke anaweza kufika kileleni zaidi ya mara moja muda mfupi tu tangu alipofika kileleni mara ya kwanza na ataendelea kupata hisia hizo endapo ataendelea kusisimuliwa, hisia hizi hudumu kwa sekunde 15 hadi 60.

Mwanamke kufikishwa kileleni na kuridhika ni jambo ambalo linahitaji ushirikiano na kuelewana kwa wenza wawili wanaoshiriki tendo hilo hasa katika maandalizi ya awali.

Tafiti zinaonyesha asilimia 10 hadi 15 ya wanawake duniani hawajawahi kufika kileleni (orgasm).

Kutofika kileleni kwa mwenza yeyote ni moja ya mambo yanayochangia migogoro isiyo na lazima kwani hudhani kuwa mwenzake siyo waaminifu katika uhusiano wao.

Kufika kileleni kwa baadhi ya wanawake huambatana na kutoa maji maji yanayosukumwa toka kwenye sehemu zake za siri kwa kasi. Maji maji haya huwa siyo haja ndogo kama inavyodhaniwa mitaani.

Kwa kawaida maji hayo hutokea ndani ya tezi ambayo mdomo wake upo jirani na tundu la njia ya haja ndogo.

Tezi hiyo inaitwa tezi ya Skene kwa lugha ya kitaalamu, ndani yake huwa na majimaji meupe.

Ufafanuzi huu utakuwa umewapa jibu kwa wale ambao huniuliza mara kwa mara kuhusiana na jambo hili.

Kwa upande wa wanaume, kufika kwao kileleni huambatana na kupata hisia nzuri za kipekee na kutoa majimaji mazito ambayo yana mbegu za kiume.

Hisia hizi huweza kudumu kwa sekundi 6 hadi 30 na huwa ni mara moja tu na si mfululizo kama ilivyo kwa mwanamke.

Kwa mwanaume, huhitaji muda kidogo ila kuamsha hisia na kuendelea na tendo na kufikia kileleni tena.

Wapo baadhi ya wanaume baada ya kufika kileleni katika mzunguko wa kwanza wanakuwa na uwezo wakuunganisha kwenda mzunguko wa pili bila kuhitaji mapumziko mafupi na kufika kileleni kwa mara ya pili.

Ili kufikia kileleni mara nyingi mtu hutumia nguvu nyingi. Na nguvu anayopoteza mwanaume kwa mshindo mmoja tu unaweza kuitumia kukimbilia kilomita kumi. Ni vizuri wenza wanapoona kuna hali isiyo ya kawaida wafanyapo tendo la ndoa, ni vema wakahi kufika katika huduma za afya kwa ushauri na matibabu.

Katika makala zijazo tutaona matatizo yanayoingilia na kusababisha matatizo ya kutofika kileleni.

No comments:

Post a Comment