Ushauri wa Chemical kwa Alikiba baada ya kuoa - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 19 April 2018

Ushauri wa Chemical kwa Alikiba baada ya kuoa


Baada ya msanii Alikiba kuoa, msanii mwenzie Chemical ametoa ushauri kwa muimbaji huyo wa ngoma ‘Seduce Me’.


Chemical akipiga story na Clouds Tv amesema Alikiba kama alivyoweka mahusiano yake siri hadi kufikia hatua ya kuoa, afanye hivyo hadi kwenye maisha ya ndoa.
“Namshauri aendelee kufanya mahusiano yake private kama alivyofanya kwa sababu maisha ya ndoa ukiyaweka wazi sana yanakuja kukuumiza. Kama alivyoamua kuweka hivyo person basi aendelee hivyo hivyo ili mradi waelewane ampende mke wake, yeye ni star mkubwa,” amesema.
Msanii Alikiba amefunga ndoa na mpenzi wake, Aminah Rikesh leo April 19, 2018 mjini Mombasa nchini Kenya. Taarifa kutoka Kenya zinaeleza kuwa wawili hao walianza mahusiano mwaka 2016.

No comments:

Post a Comment