UJIO WA UJUMBE WA WAGENI KUTOKA NCHINI YA IRAN KUIMARISHA MASHIRIKIANO ZANZIBAR - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 19 April 2018

UJIO WA UJUMBE WA WAGENI KUTOKA NCHINI YA IRAN KUIMARISHA MASHIRIKIANO ZANZIBAR

Related image
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAISI KATIBA ,SHERIA UTUMISHI WA UMMA NA
UTAWALA BORA HAROUN ALI SLEMAN AMESEMA UJIO WA UJUMBE WA WAGENI KUTO
KA NCHINI  YA  IRAN UTAENDELEA KUIMARISHA MASHIRIKIANO YALIOPO KATI YA
WANANCHI WA  ZANZIBAR NA NCHI HIYO SAMBAMBA NA KUONGEZA KASI YA
MAENDELEO.
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA MARA BAADA YA UTAMBULISHO WA UBALOZI HUO
AMESEMA AMESEMA AMEFURAHISHWA  NA UJIO WAGENI KATIKA WIZARA YAKE NA
KUELEZA KUA WIZARA HIYO INASIMAMIA NA KUSHUHULIKIA MASUALA MBALI MBALI
YA SHERIA NA UTAWALA BORA HAPA NCHINI  .
AIDHA AMEELEZA KUWA OFISI YA MWANA SHERIA MKUU NDIO INAYO SHUHULIKIA
NA KUSIMAMIA MASUALA MBALIMBALI YA SHERIA PAMOJA NA KUSIMAMIA UTUMISHI
WA UMMA.


KWA UPANDE WAKE BALOZI WAIRAN NCHINI TANZANIA DR ARDESHIR NOORIAN
AMESEMA KUWA TANZANIA NA IRAN  INA UHUSIANO WAO NA URAFIKI NI WA MUDA
MREFU AMBAPO AMEELEZA KUA UJIO WAO NI ISHARA NJEMA YA KUIMARISHA
UHUSIANO WAO ULIOPO KATI YA NCHI HIZO MBALI.
HATA HIVYO BALOZI NOORIAN AMEEZA KUA WANACHUKIZWA SANA KUONA NCHI ZA
KIISLAM WANAZIKANDAMIZA NCHI ZA WAISLAMU WENZAO ,HIVYO AMESEMA
ANAIMANI KUA UHUSIANO KATI YAO NA NCHI YA ZANZIBAR UTAWEZA KUCHANGIA
KWA KIASI KIKUBWA KUSAIDIA WAISLAMU WA MATAIFA MBALIMBALI DUNIANI
KUNUFAIKA.
SAMBAMBA  NA HAYO BALOZI HUYO AMESEMA KATIKA ZIARA YAKE AMEPATA FURSA
YA KUZUNGUMZA NA WABUNGE NA WAWAKILISHI, KATIKA KUKUZA UHUSIANO  WAO
AMEAHIDI KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA KIELIMU ,AFYA ,UTALII NA
KILIMO .NA ISHRAA SEIF

No comments:

Post a Comment