KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi Asha Ali Abdalla amesema mpango wa ugatuzi wa madaraka kutoka serikali kuu kwenda serikali za mitaa imesaidia kuboreka kwa utoji wa huduma za afya kwa wananchi . - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 17 April 2018

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi Asha Ali Abdalla amesema mpango wa ugatuzi wa madaraka kutoka serikali kuu kwenda serikali za mitaa imesaidia kuboreka kwa utoji wa huduma za afya kwa wananchi .

Image result for Bi Asha Ali Abdullah

KATIBU  Mkuu  Wizara ya Afya Zanzibar Bi Asha Ali Abdalla amesema

mpango wa ugatuzi wa madaraka kutoka serikali kuu kwenda  serikali za
mitaa imesaidia kuboreka kwa utoji wa huduma za afya kwa wananchi .Amesema tangu Serikali ianze kutekeleza mpango huo , huduma za msingi
zimeimarika na hivyo kuwafanya wananchi kuzipata kupitia Halmashauri
na Mabaraza ya Miji.Akizungumza na wakurungezi  wa Halmashauri na Mabaraza ya Miji Pemba
na watendaji  wa  Wizara ya Afya kisiwani hapa katika ukumbi wa
maabara ya afya ya jamii  Wawi Chake Chake amewaagiza wakurugenzi
kuandaa mipango kazi ambayo itaendana na misingi ya utoaji wa huduma
za afya . Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi , Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa ,
serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Kai Bashir Mbarouk amewataka
watendaji wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii ili lengo la Serikali
la kutoa huduma bora kwa wananchi liweze kufikiwa .Mwezeshaji wa kikoa hicho amewataka watendaji wanapopanga mipango yao
ya maendeleo kuhakikisha wanazifahamu huduma za msingi amazo
zinatolewa kwenye vituo vya msingi ambavyo vimegatuliwa .Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba Bi Shadia Seif  amewataka
watendaji hao kushirikiana kwa pamoja ili lengo liliokusudiwa liweze
kutekelezwa la kuafikishia huduma wananchi.

No comments:

Post a Comment