Torres afikisha magoli 100 ‘La Liga’ - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 17 April 2018

Torres afikisha magoli 100 ‘La Liga’


MSHAMBULIAJI, Fernando Torres, alifunga goli lake la 100 kwenye ‘La Liga’ wakati Atletico Madrid ikiichapa Levante huku akitangaza anaweza kuondoka majira ya joto.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea mwenye umri wa miaka 34 ambaye hajumuishwi kwenye kikosi cha kwanza msi mu huu, alifunga goli hilo akiwa umbali wa yadi 10.
Angel Correa na Antoine Griezmann walifunga magoli mawili ya kwanza ya Atletico.
Miamba hiyo iliyofuzu nusu fainali ya Ligi ya Europa inaendelea kubakia ya pili,pointi 11 nyuma ya Barcelona.
Atletico ambayo imeshinda mechi zake zilizopita 10 nyumbani na kuruhusu goli moja pekee itaivaa Arsenal kwenye mechi zitakazopigwa Aprili 26 na Mei 3.(AFP).

No comments:

Post a Comment