Timu ya vijana ya Zanzibar U17 yalimwa faini ya dola za Kimarekani 15,000 kwa kupeleka vijeba - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 17 April 2018

Timu ya vijana ya Zanzibar U17 yalimwa faini ya dola za Kimarekani 15,000 kwa kupeleka vijeba

Timu ya taifa ya vijana waliyo na umri chini ya miaka 17 ya Zanzibar, (Karume Boys) imetupwa nje ya michuano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge Cup U17 ) inayoendelea nchini Burundi baada ya kupeleka wachezaji waliyozidi umri.
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye hapo jana siku ya Jumatatu ya Aprili 16 amekiambia chombo cha habari cha Xinhua kuwa walifikia maamuzi ya mwisho siku ya Jumapili baada ya kugundua Zanzibar ilikiuka sheria za mashindano kwa kusajili wachezaji wasiostahiki.
“Zanzibar imewakilisha wachezaji waliyozidi umri kwenye mchezo wa ufunguzi wa kundi B  dhidi ya Sudan siku ya Jumapili. Mchezo ambao haukuchezwa na ndipo likagundua wachezaji wake 12 wamezaliwa kabla ya Januari 1 mwaka 2002, ambao wazi wamezidi umri unaotakiwa wa miaka 17,” amesema Musonye.
Timu ya Zanzibar imerudishwa nyumbani na kutakiwa kulipa faini ya Dola za Kimarekani 15,000 na kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la kupeleka wachezaji waliozidi umri.
Musonye ameongeza kuwa ” Fedha hizo zitapelekwa kwenye Shirikisho la soka la Kimataifa (IFA) ambao wao ndiyo wafadhili wa michuano hiyo ya CECAFA na kuitaka Zanzibar kutoshiriki michuano yote inayosimamiwa na Shirikisho hilo la Afrika Mashariki na Kati mpaka pale watakapo maliza kulipa faini.”
Wakati huo huo CECAFA ikiwaondoa wachezaji watatu wa Ethiopia na kuwarudisha nyumbani.
Michuano ya CECAFA Challenge Cup U17 inaendelea nchini Burundi na Zanzibar inadaiwa kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya Januari 1 mwaka 2002, ambao wazi wamezidi umri unaotakiwa wa miaka 17.
Na ndugu zao timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania Bara, (Serengeti Boys) ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda kwenye mechi yake kwanza ya michuano hiyo siku ya Jumapili huku wenyeji Burundi ikipoteza kwa mabao 4 – 0 mbele ya Kenya mchezo uliyopigwa Jumamosi.

No comments:

Post a Comment