Timu ya soka ya wachezaji wa zamani wa Zanzibar (Zanzibar All Star) yamuomba Rc Ayoub kuelimisha wadau wa michezo juu ya kumbu kumbu zao - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 15 April 2018

Timu ya soka ya wachezaji wa zamani wa Zanzibar (Zanzibar All Star) yamuomba Rc Ayoub kuelimisha wadau wa michezo juu ya kumbu kumbu zao


MKOA WA MJINI MAGHARIBI 
                                                                                             
Timu ya soka ya wachezaji wa zamani wa Zanzibar (Zanzibar All Star) imemuomba Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud kusaidia kuwaelimisha wadau na mamlaka za michezo juu ya umuhimu wa kutunza kumbukumbu zao.
Akizungumza wakati uongozi wa timu hiyo ulipokwenda kumshukuru Mkuu huyo na kumkabidhi kikombe cha ushindi wa Karume Day,Katibu mkuu wakikosi hicho Nd Salum hamduni,amesema inasikitisha kuona wanasoka walioiletea sifa Zanzibar hawasaminiwa hata kwa kutakiwa ushauri.
Amesema kuwa tafauti na nchi nyengina Zanzibar haina utaratibu wa kutunza historia za wanamichezo wake wa zamani ambao waliiwakilisha Zanzibar kimataifa na kuifanya itambulike na kuheshimiwa ndani na nje ya nchi.
Nd Hamduni amemuomba Mkuu wa Mkoa atumie nafasi yake kuhakikisha wanamichezo wa zamani wanapewa hadhi na heshima ya kushirikishwa katika baadhi ya mambo ya kitaifa,ikiwemo kusikilizwa maoni yao wakati wa kuunda timu za taifa hususani mpira wa miguu.
Ameongeza kuwa wao wamecheza mpira zamani na kwa kiasi kikubwa wamesaidia nchi yao ya Zanzibar kufahamika kimichezo na kuheshimiwa,Hivyo kwa vyovyote vile wanazo fikra,mipango na maarifa yanayoweza kusaidia katika jitihada za kuendeleza michezo kama nchi nyengine zinavyowapa umuhimu veteran wao na na hata kuwaalika kwenye mashindano makubwa yakiwemo ligi ya Mashindano ya Mapinduzi.
Katibu Hamduni alielezea kusikitishwa kwao na namna watu waliopewa dhamana ya kuongoza vyama vya michezo hasa mpira wa miguu wanavyochukulia wazee kuwa ni maadui badala ya kuwaweka karibu kwa ajili ya kuchota  uzoefu na maarifa katika kupeleka mbele sekta ya michezo nchini.

Mapema kocha Mkuu wa timu hiyo Nd Abdallah  Maulid amemuopmba Mkuu wa Mkoa kuwakutanisha wadau na mamlaka za michezo ili kujadili namna wanavyoweza kunufaika na mchango wa wanamichezo wa zamani kwa lengo la kurejesha hadhi ya michezo nchini.
Alishauri hata wakati wa mashindano ya kombe la Mpinduzi kuandaliwe mchezo maalum ama siku ya ufunguzi au fainali utakaowakutanisha wakongwe wenzao wa Tanzania Bara ili kuwafanya vijana wa sasa kuwatambua watangulizi wao na kuona umuhimu wa kucheza mpira wa miguu.
Nae Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud pamoja na kukubali kuwa mlezi wa Zanzibar Old Stars,ameahidi kufanya kila juhudi kuhakikisha timu hiyo inaimarika na kuweza na kuwa alama nzuri ya michezo visiwani Zanzibar.
Amesema kuwa miongoni mwa majukumu yake,ni kuhakikisha agizo la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein la kurejesha vuguvugu la michezo nchini linatekelezwa na kufanikiwa.
Mapema,kaim nahodha wa Timu hiyo Ali Sharifu Adolph alimkabidhi Mkuu wa Mkoa kikombe walichokipa baada ya kuicha timu ya Young Africans Veterans mabao 2-1 katika mchezo wa maadhimisho ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume uliochezwa April 8,2018 katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Mkuu huyo bwa Mkoa ndie alieyedhamini safari ya timu hiyo kwenda Dar es Salaam ambayo imeasisiwa mwaka 2009 kwa ajili ya kuwaunganisha wanandinga hao na kuiwekea Zanzibar historia kisoka.

NA MZEE GEORGE

No comments:

Post a Comment