TETESI: Mourinho kumuuza Pogba na mastaa wengine watatu mwishoni mwa msimu - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 17 April 2018

TETESI: Mourinho kumuuza Pogba na mastaa wengine watatu mwishoni mwa msimu


Kocha wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho yupo tayari kumuachia kiungo wake ghali zaidi, Paul Pogba kuondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Pogba amedaiwa kutokuwa na mawasiliano mazuri na Mourinho tangu kuanza kwa msimu huu huku mara kadhaa akionekana kukaa benchi na nafasi yake kuchukuliwa na kinda Scott McTominay.
Kiungo huyo alisajiliwa kwa mara ya pili na Man United mwaka 2016 kwa kiasi cha paundi milioni 86 akitokea Juventus huku usajili huo ukiweka rekodi ya dunia kwa kipindi hicho.
Wakati huo huo wachezaji wengine wa United ambao wametajwa kutaka kuondoka mwishoni mwa msimu huu ni Anthony Martial, Daley Blind na Matteo Darmian.

No comments:

Post a Comment