TANZIA: Tasnia ya muziki wa Bongo Fleva yapata pigo, Msanii Jebby afariki dunia - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 22 April 2018

TANZIA: Tasnia ya muziki wa Bongo Fleva yapata pigo, Msanii Jebby afariki dunia

Msanii wa Bongo Fleva, Jebby ambaye amewahi kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Swahiba’ amefariki dunia leo April 22, 2018 mjini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na Bongo5 mjomba wa marehemu Jebby aliyejitambulisha kwa jina moja la Julius, amesema Jebby  alikuwa anasumbuliwa na Bandama mpaka umauti umemkuta.
Wimbo wa Swahiba ulifanya vizuri miaka ya 2007/9 na wimbo huo alimshirikisha rapa Afande Sele na tayari Afande ameshatoa salamu zake za rambi rambi kufuatia msiba huo.
Hayupo tena duniani SWAHIBA…Pumzika kwa amani mdogo wangu Jebby…Tukimaliza kazi tutavalishwa Taji“ameandika Afande Sele kwenye ukurasa wake wa Instagram.

No comments:

Post a Comment