TANZIA: Straika wa timu ya taifa ya vijana Malawi, Abel Mwakilama afariki dunia - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 22 April 2018

TANZIA: Straika wa timu ya taifa ya vijana Malawi, Abel Mwakilama afariki dunia


Straika wa timu ya taifa ya vijana ya Malawi, Abel Mwakilama amefariki dunia hapo jana siku ya Ijumaa Aprili, 20 huko nchini Ureno huku chanzo cha kifo chake kikitajwa kuwa ni Malaria.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Malawi (FAM), Alfred Gunda amethibitisha kifo cha mchezaji huyo aliyekuwa akikipiga kwenye timu ya Sporting Clube de Esmoriz huko Urerno kupitia mtandao wa CAFonline.com
Kupitia mtandao huo Gunda amesema kuwa wameshitushwa na taarifa hiyo na kuuzunika.
“Tumeshitushwa na kuuzunishwa sana na taarifa hiyo ,” amesema, Gunda.
Mwakilama aliiwezesha timu yake ya zamani ya Chitipa United kupanda ligi kuu ya nchini Malawi (TNM Super League) mwaka 2017 baada ya kuifungia jumla ya mabao 35 msimu wa 2016.

No comments:

Post a Comment