Tanzania yapanda nafasi 9 viwango vya FIFA - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 15 April 2018

Tanzania yapanda nafasi 9 viwango vya FIFA


Tanzania imepaa kwa nafasi 9 hadi nafasi ya 137 kutoka nafasi ya 146 kati ya mataifa 211 katika viwango vya ubora wa soka duniani vilivyotolewa na FIFA siku za hivi karibuni.
Taifa Stars kwa siku za hivi karibuni imekuwa ikicheza katika kiwango kizuri ambapo iliwashinda DR Congo katika mchezo wa kirafiki kwa mujibu wa ratiba za FIFA.
Katika viwango hivyo vipya vya mwezi Aprili, Germany imeendelea kushika nafasi ya kwanza kwa dunia huku Brazil ikiwa nafasi ya pili na Ubelgiji imefanikiwa kupanda nafasi mbili juu na kufikia nafasi ya tatu.
Katika kumi bora mataifa yanayofuata ni Ureno, Argentina,Uswiss, Ufaransa, Hispania, Chile na Poland inakamata nafasi ya 10.
Aidha, Barani Afrika Tunisia inaongoza ikiwa nafasi ya 14 ikifuatiwa na Senegal katika nafasi ya 28, Congo DR nafasi ya 38, Morocco nafasi ya 42, Nigeria nafasi ya 47, Cameroon nafasi ya 51, huku Burkina Faso akiangukia nafasi ya 53.
Hata hivyo, kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda imepanda juu nafasi nne mpaka kufikia 74, ikifuatiwa na Kenya ikiwa imeporomoka kwa nafasi 8 hadi kufikia 113, Rwanda nayo ikiporomoka kwa nafasi 11 hadi kufikia 123, Tanzania ikiwa imepanda nafasi 9 hadi kufikia 137, Ethiopia ikiporomoka kwa nafasi 8 mpaka kufikia 145 huku Burundi ikidondoka kwa nafasi 3 na kufikia 145.
Wengine ni Djibouti ambayo iko nafasi ya 198 huku Eritrea na Somalia zikiwa mkiani kabisa katika nafasi ya 206

No comments:

Post a Comment