Taarifa rasmi kutoka Arsenal kuhusiana na Arsene Wenger - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 22 April 2018

Taarifa rasmi kutoka Arsenal kuhusiana na Arsene Wenger

“Baada ya majadiliano ya muda sasa na klabu yangu nona mwisho wa msimu huu nitaachia ngazi, ninashukuru na naona fahari kwangu kuitumikia klabu kama hii kwa miaka mingi na yenye kumbukumbu nyingi”
“Niliitumikia klabu hii kwa kujitoa sana na kwa moyo wangu wote, na ningependa kuwashukuru viongozi wa timu pamoja na wafanyakazi wenzangu ambao wanaifanya klabu hii kuwa ya kipekee zaidi”

“Ningewataka mashabiki wa klabu hii waendelee kuiunga mkono timu hii ili iendelee kuwa juu, na waendelee kuithamini timu hii, hakika mapenzi yangu katika timu hii yatakuwa milele na milele” Arsene Wenger.

Hiyo ndio taarifa kubwa zaidi ulimwenguni kwa sasa na huo ndio ujumbe wa Arsene Wenger kwenda kwa mashabiki wa Arsenal baada ya hii leo kutangaza rasmi kung’atuka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Stan Kroenke “ni siku ngumu sana kwa upande wetu, kuanzia ndani mpaka nje ya uwanja Wenger amekuwa na sisi na msaada wake katika klabu hii hauwezi kuelezeka wala kufananishwa na kitu chochote”

“Tunashukuru kwa kila kitu na kila mpenda soka lazima atakuwa anakubali kwamba Wenger ni bora, tunashukuru kwa makombe yote aliyotupa na rekodi ya kucheza msimu mzima bila kupoteza” hayo ni maneno ya mmiliki mkubwa wa hisa za Arsenal Stan Kroenke.

No comments:

Post a Comment